Breaking

Saturday 13 August 2022

TENGENI MAENEO YA MALISHO KUEPUSHA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI



Na Lucas Raphael,Tabora

Halmashauri za mikoa ya Tabora na kigoma zimetakiwa kutenga maeneo ya malisho kwa ajili ya wafugaji kwa lengo la kuepusha migogoro kati ya wakulima na wafugaji wa mikoa hiyo.

Kauli hiyo ilitolewa August 11, 2022 na Afisa malisho kutoka wizara ya mifugo na uvuvi, Emmanuel Kato alipokuwa akifanya mahojiano na mwandishi wa habari hizi kwa lengo la kutaka kujua vipi migogoro ya wakulima na wafugaji itakavyoweza kumalizwa na wizara husika .

Alisema kwamba kutokana na maeneo kuwa ni ndogo hakuna budi halmashuari katika za mikoa hiyo kutenga maeneo hayo ambayo yapo ila bado hawajatenga kwa ajili ya kilimo na mifugo.

Alisema kwamba halmashauri nyingi nchini hazijatenga maeneo kwa ajili ya malisho ya mifugo na badala yake maeneo ya vijiji ndio yanatumika kwa makazi na kilimo .

Alisema jambo hilo ndilo linalosababisha kutomalizika kwa migogoro baina ya wafugaji na wakulima kwa sababu ya wafugaji kulishia kwenye mashamba ya wakulima

“Ria yangu kwa halmashauri za mikoa hii miwili Tabora na kigoma hazijafanya hivyo ziweze kutenga maeneo kwa ajili ya malisho na ikiwezekana maeneo yote yaliyokwisha tengwa na yatayotengwa yapimwe na yaweze kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali ili wafugaji waweze kuyamiliki kisheria kwa kufanya hivyo tutaweza kuondokana kabisa na migogoro isiyo ya lazima “alisema Kato

Hata hivyo afisa huyo wa malisho kutoka wizara ya mifugo na Uvuvi aliwataka wafugaji kutunza malisho ya ziada kwa ajili ya kupambana na kiangazi kirefu na kufuga mifugo michache yeye tija .

Emmanuel Kato alisema kwamba kwa mwaka huu wa fedha wizara ya mifugo imejipanga kuboresha sekta ya mifugo kwa kuchimba mabwawa na malambo na visima virefu ili kuhakikisha mifugo na wafugaji wanakuwa na maji ya kutosha ya uhakika kwa mwaka mzima .

Alisema lengo lingine la wizara ni kuhakikisha wanajenga mnada ya awali ni ile inayosimaniwa na halmashauri za wilaya , upili ni mnada inayosimami na wizara ya mifugo na uvuvi na mipakani ni mnada iliyomikapani mwa nchini na kusimamiwa na wizara husika kwa kukasimiwa majukumu yake na halmashuari ya wilaya iliyokaribu na mpaka wa nchi jirani.

mwisho.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages