Breaking

Sunday 6 November 2022

ABIRIA 26 WAOKOLEWA AJALI YA NDEGE KAGERA



Mkuu wa Mkoa wa Kagera Albert Chalamila amesema Ndege ya Precision Air iliyopata ajali wakati wa kutua Bukoba leo ilikuwa imebeba Watu 43 ambapo hadi sasa wameokolewa 26 tu na kupelekwa hospital ya Rufaa ya mkoa Kagera.

Japo Mkuu wa Mkoa hajasema Watu hao waliokolewa vipi na muda gani, Mashuhuda wanasema huenda waliokolewa sekunde chache baada ya ajali kabla sehemu kubwa ya Ndege hiyo kufunikwa na maji, tunaendelea kufuatilia zaidi ili kupata taarifa kamili kutoka kwa Mamlaka.

Soma Pia: AJALI YA NDEGE KAGERA, RAIS SAMIA AWAASA WATANZANIA KUWA WATULIVU

Kwa upande mwingine RC Chalamila amewaomba Wananchi kuendelea kuwa watulivu maana mawasiliano na Marubani walioko ndani ya ndege bado yanaendelea.

Ndege hiyo ni ATR 42 yenye namba za usajili 5H BWF ambayo ilikua ikitokea Dar es salaam kuelekea Bukoba na ilikua na safari ya kurudi Dar es salaam kupitia Mwanza.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages