Breaking

Sunday 6 November 2022

AJALI YA NDEGE KAGERA, RAIS SAMIA AWAASA WATANZANIA KUWA WATULIVU


Na Samir Salum, Lango la habari

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kufuatilia ajali ya Ndege ya Kampuni la Ndege la Precision Air kuanguka katika Ziwa Victoria baada ya kushindwa kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Bukoba Mkoani Kagera.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Rais Samia amethibitisha kupokea taarifa ya ajali hiyo na kuongeza kuwa "Natuma salamu za pole kwa wote walioathirika na ajali hii"


Aidha amewataka watanzania kuwa watulivu wakati zoezi la uokoaji likiendelea.

"Tuendelee kuwa watulivu wakati huu zoezi la uokoaji likiendelea huku tukimuomba Mwenyezi Mungu atusaidie" amesema Rais Samia 


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera William Mwampaghale amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo leo jumapili Novemba 06, 2022 na kuwa juhudi za uokoaji zinaendelea kufanywa na Zimamoto, JWTZ pamoja na wavuvi.


Taarifa zaidi kukujia hivi punde!


Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages