Breaking

Wednesday 16 November 2022

AKAMATWA KWA KUJIFANYA POLISI



Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linafuatilia kundi la Watu wanaojifanya ni Askari Polisi wakati mwingine Maafisa wa Usalama wa Taifa ambao hukamata Watu hovyo, kuzunguka nao mitaani kwa kutumia gari huku wakiwatishia juu ya tuhuma mbalimbali za uongo na baadae kuwataka watoe pesa ndio wawaachie.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Muliro Jumanne amesema katika ufuatiliaji wa suala hilo amekamatwa Joseph James (32) Mkazi wa Kijitonyama ambaye amekuwa akijifanya ni Askari Polisi kutoka Ofisi ya Upelelezi Makao Makuu ya Polisi Dodoma.

"Uchunguzi umebaini, mtuhumiwa huyu amekuwa akishirikiana na wenzake ambao wamekuwa wakitumia gari aina ya Subaru lenye namba za usajili T 550 DST alilokamatwa nalo mtuhumiwa huyo" Ameeleza Kamanda Muliro 

Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam linaendelea kuwasaka wahalifu wote wanaofanya utapeli wa namna hii ili wakamatwe na kufikishwa kwenye mifumo ya kisheria kwa hatua zaidi.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages