Breaking

Wednesday 16 November 2022

JAMAA AIBA MILIONI 60 ZA WACHINA KISHA AJITEKA



Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Deodatus Luhela (35) maarufu baba banzi mhasibu wa Kampuni ya kichina iitwayo ‘‘YOUR HOME CHOICE’ iliyopo Keko kwa uhuma za uongo akidai kuvamiwa na majambazi na kuporwa Milioni 60.

Akitoa taarifa leo Jumatano Novemba 16, 2022 Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam ACP Jumanne Muliro amesema kuwa mnamo Tarehe 14/11/2022 eneo la Chang’ombe Temeke, Dar es Salaam alikamatwa Deodatus kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo kituo cha Polisi huku akidai kuwa majambazi walimjeruhi na kumpora Tsh 60,000,000 alizo kuwa ametumwa na mwajiri wake kuzichukua kutoka benki ya CRDB Tazara.

 
 Kamanda Muliro ameeleza kuwa Mtuhumiwa huyo alidai tarehe hiyo majira ya saa 3:30 asubuhi alikamatwa na majambazi wawili waliokuwa na gari nyeusi baada ya kumtishia kwa silaha baadae akaingizwa kwenye gari ambapo walimjeruhi mkono wa kushoto na shavuni, na kumpora fedha alizokuwa nazo.

 " alidai kuwa walimtupa maeneo ya Gongo la Mboto njia panda ya Pugu na Mbezi alijikongoja hadi kituo cha Polisi kidogo cha Gongo la Mboto ambako alipewa PF. 3 kwaajili ya matibabu" 

Baada ya tukio hilo majira ya saa 8 :00 mchana mtuhumiwa huyo alifungua kesi kituo cha Polisi Chang’ombe ya unyang’anyi na kuporwa tsh 60,000,000.

"Makachero wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam walimuhoji kwa kina na kubaini kuwa taarifa hizo zilikuwa ni za uongo na ilipofika tarehe 15/11/2022 majira ya saa 8 :00 mchana mtuhumiwa aliwaongoza askari hadi Chanika Kitunguu alipokuwa amezificha pesa hizo" ameeleza Kamanda Muliro

Aidha Kamanda Muliro ametoa onyo kwa wananchi juu ya tabia ya kutoa taarifa za uongo kwa maafisa wa Serikali kuwa ni kosa na ikibainika watachukuliwa hatua stahiki kwa mujibu wa sheria ikiwa ni pamoja kufikishwa mahakamani.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages