Breaking

Wednesday 2 November 2022

MAWAKALA WATANO WAKAMATWA KWA KUSAJILI LAINI ZA SIMU WAKITUMIA NIDA ZA WATU WENGINE



Na Lydia Lugakila,Kagera

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU)Mkoa wa Kagera kupitia ufuatiliaji wake wamebaini na kuwakamata mawakala 5 wa kampuni za simu za mikononi wasio waaminifu huku uchunguzi zaidi ukiendelea ili hatua zichukuliwe dhidi yao.

Akitoa taarifa ya utendaji kazi wa taasisi hiyo katika kipindi cha miezi 3 kwa waandishi wa habari Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Kagera John Joseph amesema kuwa wamefanikiwa kuwakamata mawakala 5 wa kampuni za simu za mikononi wasio waaminifu ambao wamekuwa wakiwasajilia laini za siku  wananchi kwa kutumia 
namba ya NIDA na majina ya watu wengine huku baadhi ya namba hizo kutumika katika uhalifu.

"Nashauri wananchi nendeni kwa viongozi wa makampuni ya simu ngalia kama line zenu zimesajiliwa kwa namba ngapi kwani kuna uwezekano namba yako ya NIDA ikawa imetumika kusajili laini zaidi ya moja hivyo ukibaini hali hiyo toa taarifa zifutwe au zifungwe ili kuepusha uhalifu alisema mkuu wa TAKUKURU"

Ameongeza kuwa taasisi hiyo imekamatwa laini 5 ambazo zimekuwa zikisajili kwa kutumia majina ya watu wengine huku akiongeza kuwa mara nyingi mawakala batili hutumia njia "rudia tena" ili wachukue alama za vidole na kisha kusajilia wengine.

Joseph amesema kuwa ni vyema kila mtu anapokwenda kusajili line yake ya simu awe makini kwani wamebaini namba hizo zimesajiliwa kwa kutumia majina ya watu wengine, huku akieleza kuwa mara nyingi ukifuatilia utaona picha za watu walio wengi ni wale waliokwisha fariki dunia.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages