Breaking

Wednesday, 2 November 2022

WAZIRI MKUU ATOA MAAGIZO KWA DAWASA


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akishika maji mara baada ya kuzindua maji kwa ajili ya wakazi wa Kigamboni na Dar es Salaam alipotembelea mradi wa maji wa Kisarawe II uliopo Kigamboni ili kujionea maendeleo ya mradi huo ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia Suluhu ya kuhakikisha maji ya Kigamboni yanafika Dar es Salaam ili kupunguza makali ya mgao wa maji. (Via Michuzi)

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akifungua koki ya maji kuashiria uzimduzi wa maji wa Kisarawe II kwa ajili ya wakazi wa Dar es Salaamwakati wa ziara yake ya kukagua mradi wa maji wa Kisarawe II uliopo Kigamboni ili kujionea maendeleo ya mradi huo ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia Suluhu ya kuhakikisha maji ya Kigamboni yanafika Dar es Salaam ili kupunguza makali ya mgao wa maji.
Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza kuhusu namna wanavyoendelea na jitihada za kupunguza ukali wa mgao kwa kuhakikisha wanapeleka maji Dar es Salaam kwa kutumia mradi wa maji wa Kisarawe II uliopo Kigamboni wakati wa ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ya kukagua maendeleo ya mradi huo Pamoja na kuzindua maji yatakayotumika Mkoa wa Dar es Salaam.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla akizungumza kuhusu kupokea maagizo aliyopewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa alipokagua maendeleo ya mradi wa maji wa kukagua ujenzi wa Tanki, uchimbaji wa visima kwenye mradi wa maji wa Kisarawe II katika Wilaya ya Kigamboni Mkoani Dar es Salaam.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa moja ya visima vinavyozalisha maji kwenye mradi wa Kisarawe II wakati wa ziara ya kukagua mradi wa maji wa Kisarawe II uliopo Kigamboni jijini Dar es Salaam ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha wakazi wa Dar es Salaam wanapata maji kutoka kwenye mradi huo.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso pamoja na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla wakipata maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja kuhusu mradi wa Kisarawe II walipotembelea Tanki la maji la Kisarawe II lenye ujazo wa Lita Milioni 15 linalojengwa na DAWASA lililopo Wilaya ya Kigamboni Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya kukagua mradi wa maji wa Kisarawe II hii ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia Suluhu.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akizungumza jambo mara baada ya kupata maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja kuhusu mradi wa Kisarawe II walipotembelea Tanki la maji la Kisarawe II lenye ujazo wa Lita Milioni 15 linalojengwa na DAWASA lililopo Wilaya ya Kigamboni Jijini Dar es Salaam

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi pamoja na waandishi wa habari wakati wa kutembelea mradi wa maji wa Kisarawe II uliopo Kigamboni ili kujionea maendeleo ya mradi huo ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia Suluhu ya kuhakikisha maji ya Kigamboni yanafika Dar es Salaam ili kupunguza makali ya mgao wa maji.


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso pamoja, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama wakiendelea na ziara ya kukagua mradi wa maji wa Kisarawe II uliopo Kigamboni jijini Dar es Salaam ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha wakazi wa Dar es Salaam wanapata maji kutoka kwenye mradi huo. (Via Michuzi)

Pages