Breaking

Thursday 17 November 2022

NDEGE YA ATCL YASHINDWA KUTUA BUKOBA



Ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) imeshindwa kutua katika uwanja wa ndege wa Bukoba mkoani Kagera kutokana na hali mbaya ya hewa.

Badala yake ndege hiyo imelazimika kutua salama katika uwanja wa Mwanza

Alipoulizwa kwa simu leo Alhamisi Novemba 17 kuhusu tukio hilo, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Hamza Johari amethibitisha tukio hilo.

“Ni kweli nimepata taarifa ndege ya Air Tanzania imeshindwa kutua kutokana na hali mbaya ya hewa, kulikuwa na ukungu, mvua, radi na giza uwanja ukawa hauonekani, kwa hiyo rubani akafuta safari na kurudi Mwanza na ametua salama,” amesema.


Awali taarifa iliyotumwa na Mbunge wa Viti Maalum, Neema Lugangira kwenye mitandao ya kijamii ilieleza tukio hilo.


“Still shaken lakini Mungu ni Mwema. Nimepanda ndege asubuhi ya leo kwenda Bukoba. Safari ilikuwa na changamoto, tumefika lakini ndege ikashindwa kutua.

“Nampongeza rubani kwa uamuzi sahihi wa kurudi Mwanza na sasa narudi Dar. Serikali ibebe kwa uzito suala la airport mpya Bukoba,” ameandika.


Hali hiyo imejitokeza zikiwa zimepita siku 11 tangu ndege ya shirika la Precision ilipoanguka katika ziwa Victoria na kusababisha vifo vya watu 19 na wengine 24 kuokolewa.


Via:Mwanachi
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages