Breaking

Monday 7 November 2022

SOKO LA MAZAO MISUNGWI HALINA CHOO ZAIDI YA MIAKA 30, MWENYEKITI WA KIJIJI ATUPIA LAWAMA HALMASHAURI



Na Paul Kayanda, Misungwi

MWENYEKITI wa Serikali ya Kijiji cha Mabuki Kata ya Mabuki Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza Selemani Masoud amesema kuwa Soko la mazao ya nafaka katika Kijiji hicho halina choo hali ambayo siyo salama kiafya.


Soko la Mabuki katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi limedaiwa kuanzishwa mwaka 1988 na ni chanzo kikubwa cha mapato ya ndani katika Halmashauri hiyo ambayo mpaka sasa Mkurugenzi wake anakusanya mapato kupitia ushuru huku soko hilo likiwa halina choo.


Amesema kuwa ukosefu wa choo katika soko hilo linalokusanya wafanyabiashara kutoka maeneo mbalimbali pamoja na umati mkubwa wa wananchi wa vijiji vya Kata mbalimbali wilayani hapa wanaokuja kupata huduma ya soko hali ya mlipuko wa magonjwa unaweza kutokea wakati wowote kutokana na uchafuzi wa mazingira.


Mwenyekiti wa serikali ya Kijiji hicho Selemani Masoud akizungumza hivi karibuni na waandishi wa Habari waliotaka kujua mkakati wa ujenzi wa choo katika Soko hilo ili kunusuru magonjwa ya mlipuko alisema kuwa Soko hilo linaonesha kuinufaisha Halmashauri pamoja na wananchi wa kijiji chake na vijiji jirani vya kata za pembezoni.


“Ndugu zangu waandishi wa Habari naninyi tusaidieni kupaza sauti ili tujengewe choo bora katika gulio letu, Gulio tunalo,wananchi wanapata faida ya kuuza mazao yao na wengine kununua lakini gulio hilo lipo chini ya Halmashauri,” alisema Masoud na kuongeza.


“Sisi kama Kijiji hatunufaiki na hili Gulio, Halmashauri wanakuja kukusanya ushuru na hakuna kiasi chochote kinachoachwa kwaajili ya maendeleo yetu na mpango tulio nao sasa kama halmashauri wataendelea kuchelewa tutatafuta wadau wa hapa hapa kijijini ili wajenge tuingie ubia nao wa kukusanya chochote kwaajili ya Kijiji,” alisema.

Pia somaABIRIA WATATU WAFARIKI AJALI YA NDEGE KAGERA

Alifafanua kuwa Soko hilo lilianzishwa tangu mwaka 1988 mpaka sasa wananchi wanafanya biasahara zao bila choo na kuongeza kuwa wakibanywa haja wanakwenda nyumba jirani ama vichakani kulingana na jiografia ya eneo lilipo soko hilo lakini ukweli kwa sasa linazungukwa na makazi ya wananchi hivyo Halmashauri waone umuhimu wa kuchimba na kujenga choo badala yake Kijiji kitaleta mdau ili nacho kipate haki yake.




Hata hivyo akizungumzia suala la ukosefu wa choo kwenye Soko hilo Diwani wa Kata hiyo Malale Lutonja Alikili kuwepo kwa changamoto hiyo kwa kipindi kilefu na kudai kuwa Halmashauri ipo mbioni kutatua kero hiyo ukilinganisha kuwa soko hilo ni sehemu ya chanzo cha mapato ya ndani.


Mwisho.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages