Breaking

Sunday 6 November 2022

VIFO VYAFIKIA 19 AJALI YA NDEGE KAGERA, WAZIRI MKUU ATOA MAAGIZO



Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameeleza kuwa abiria 19 waliokuwa kwenye ndege ya Precision Air iliyotumbukia Ziwa Victoria ilipokuwa ikikaribia uwanja wa ndege Mkoani Kagera wamefariki dunia.

''Uchunguzi ufanyike ili kujua hao wawili wanaoongezeka kwenye idadi wametoka wapi, kama ni miongoni mwa walioenda kuokoa au kama ni watumishi wa ndege hawakuandikishwa'' -  Amesema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. 


Ameeza kuwa kwa namna ndege hiyo ilivyotumbukia katika ziwa Victoria kwa kutangulizi kichwa hakuna matumaini ya rubani wa ndege hiyo kuwa hai.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Precision Air Bw. Patrick Mwanri alielezea ajali hiyo kama “janga” akitangaza vituo viwili vya habari vya Dar es Salaam na Bukoba.

Soma Pia: AJALI YA NDEGE KAGERA, RAIS SAMIA AWAASA WATANZANIA KUWA WATULIVU

Kwa mujibu wa maelezo rasmi, ndege hiyo ya abiria PW494 ilikuwa na abiria 39 na mtoto mchanga. Ndege hiyo ilitoka Dar es Salaam na ilipangwa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Bukoba na kuelekea Mwanza kabla ya kurejea Dar es Salaam Jumapili.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages