Breaking

Thursday 10 November 2022

TAMASHA LA KIMATAIFA LA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO KUANZA LEO, KUFUNGULIWA RASMI NA MAKAMU WA RAISNa John Mapepele

Tamasha la Kimataifa la 41 la Utamaduni na Sanaa Bagamoyo linaanza leo Novemba 10, 2022 mjini Bagamoyo Kwa kufanya kongamano itakalojadili kwa kina masuala ya Sanaa na uchumi litalaloongozwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa


Wadau mbalimbali wa sanaa kutoka ndani na nje ya nchi na Watendaji Wakuu wa makampuni makubwa nchini wamealikwa kuchangia katika mdahalo huo.Aidha, baada ya kongamano hilo, kutakuwa na maonesho ya kazi za Sanaa kwenye viwanja vya Chuo cha Sanaa Bagamoyo (TaSUBa) na usiku kupambwa na tumbuizo la michezo mbalimbali ya Sanaa ambapo vikundi mbalimbali vya Sanaa kutoka maeneo duniani vitapamba.

Kesho, ambayo ni siku ya pili ya Tamasha, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt, Philipo Mpango atafungua rasmi tamasha hilo ambapo usiku vikundi mbalimbali vitatumbuiza na Mgeni maalum katika usiku huo atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani.Siku ya mwisho, Tamasha litatamatishwa na burudani kali kutoka kwa wasanii mbimbali ambapo Mgeni maalum atakuwa Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Pauline Gekul.Aidha, siku ya mwisho washiriki wote watapata fursa ya kufanya Royal tour ya kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii katika mji wa Bagamoyo na kutembelea kisiwa cha Liz lagoon
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages