Breaking

Monday 16 January 2023

HOSPITALI YA WILAYA YA ITILIMA YAANZA KUTOA HUDUMA ZA UPASUAJI



OR-TAMISEMI

Hospitali ya Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu imeanza kutoa huduma za upasuaji kwa wakinamama wanaopata uchungu pingamizi.

Akizungumza Mganga Mkuu wa Wilaya ya Itilima Dkt. Anold Musiba amesema “Tumefanikiwa kuanza kutoa huduma ya upasuaji kwa kina mama wajawazito wanoshindwa kujifungua kwa njia ya kawaida kutokana na sababu mbali mbali pia tumeanzisha huduma ya watoto njiti pamoja na wale wanaohitaji uangalizi wa karibu sana baada ya kuzaliwa(NICU)”.




Pia Dkt. Anold Musiba ameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwanamna inavyojitoa kuhakikisha huduma bora za afya zinawafikia watanzania wote kokote kule waliko.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages