Breaking

Wednesday 22 February 2023

AUAWA AKIKABA WANAWAKE USIKU WA MANANE

Picha haihusiani na tukio


Mwanaume mmoja anayefahamika kwa jina la Majid Mohamed,mwenye umri wa miaka 36 Mkazi wa Tinde ameuawa kwa kushambuliwa na wananchi waliojichukulia sheria mkononi kwa tuhuma za kuwadanganya kuwa yeye ni wakala wa mabasi kisha kuwavamia na kuwaibia mali zao.


Akieleza juu ya tukio hilo Diwani wa Kata ya Tinde,Jafari Makwaya amesema tukio hilo limetokea Februari 21 2023 Majira ya saa nane usiku katika kitongoji cha Jomu Kata ya Tinde Mkoani Shinyanga, ambapo mwanaume huyo alikuwa amewavamia wanawake wawili kwa lengo la kuwaibia lakini mlinzi wa malori barabarani na madereva malori walifanikiwa kuwaokoa wanawake hao.


"Alipigwa akiwa kwenye shughuli za kuwavamia watu lakini dereva wa Lori na mlinzi wa malori walishuhudia tukio zima ambapo walienda kutoa msaada kwa wanawake wale kisha wakamvizia Majid Mohamed akiwa anakimbia kisha kumpiga na kitu chenye ncha kali na kumtupia kwenye mfereji wa barabarani", amesema Makwaya.


"Alikuwa anawadanganya watu kuwa ni wakala wa mabasi na ni mzawa wa Tinde na amewahi kufungwa kifungo cha maisha kwa kosa la ubakaji na wizi wa madawa ya hospitali na baada ya kutoka gerezani alianza kutishia maisha watu waliofuatilia kesi ,kuna idadi kubwa ya vijana ambao hawana kazi katika kata hii hivyo niombe kwa vyombo vya ulinzi na usalama kushughulika na vijana wanaowadanganya watu na kuwaibia kwa kimvuli cha uwakala", ameongeza.

Inaelezwa kuwa kijana huyo anayedaiwa kuwa kibaka maarufu amekuwa tishio katika eneo la Tinde kutokana na vitendo vyake huku wananchi wakidai amekuwa akikingiwa kifua hivyo kutofungwa jela.

Via: Malunde 1 Blog 
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages