Breaking

Wednesday 22 February 2023

RAIS SAMIA ATUMA SALAMU ZA KWARESMA, ATOA WITO



RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan amewatakia Wakristo wote Kwaresma njema.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa fupi aliyoitoa kupitia mitandao yake rasmi ya kijamii leo Februari 22, 2023 ikiwa ni Jumatano ya Majivu.

"Nawatakia Kwaresma njema Wakristo wote. Katika hija hii ya kiroho mnayoianza leo kwa Jumatano ya Majivu, endeleeni kuiombea nchi yetu na Dunia nzima amani na upendo.

"Majivu katika paji la uso yawakumbushe ubinadamu wenu na kumrudia Mwenyezi Mungu, mkiomba ulinzi wake kwetu sote,"amefafanua Rais Dkt.Samia
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages