Breaking

Tuesday 13 June 2023

BILIONI 7 KUJENGA MIUNDOMBINU UMWAGILIAJI SHAMBA LA MBEGU KILIMI

Raphael Lucas, Tabora

Serikali imetoa kiasi cha shilingi bilion 7 Kwa ajili uwekaji wa Miundombinu ya Umwagiliaji katika Shamba la Mbegu Kilimi Wilayani Nzega  mkoani Tabora kwa lengo la kuongeza uzalishaji kwa kipindi chote cha mwaka .

Kauli hiyo ilitolewa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za kilimo nchini (ASA) Dkt, Sophia Kashenge baada ya kufanya  ziara ya kukagua Mradi huo katika Shamba la Mbegu Kilimi linalowekewa miundombinu ya Umwagiliaji Kwenye eneo la Hekta 400 sawa na Ekari 1,000.

 

Alisema kwamba serikali imetoa fedha nyingi Kwa ajili ya kuongeza  uzalishaji  wa mbegu kipindi chote Cha mwaka togauti na kipindi ambacho tunatengemea mvua za masika tu.

 

Alisema kwamba uzalizaji utaongezeka kutoka tani 200 zilizikuwa zinazalishwa kwenye hekta 200 na sasa utapanda hadi kufikia tani 1000 kwenye hekta 200 na huo ni wastani wa chini wa uzalishaji .

 

Dkt Sophia kwamba shamba la mbegu  kilimi litakapo kamilika ufungaji wa miundombinu hiyo katika hekta zote 400 uzalishaji utaongeza mara dufu wa upatikanaji wa mbegu kwa  ukanda wa ziwa na Magharibi ya nchini .

 

 

Hata hivyo Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za kilimo (ASA) ameridhishwa na kazi inayoendelea ya uwekaji wa Miundombinu ya Umwagiliaji katika Shamba la Mbegu Kilimi Nzega Tabora unaofanywa na Kampuni ya Pro Agro Global ltd.

 

 

Alisema kazi hiyo imefikia asilimia 57 ambapo Mitambo ya Pivot minne kati ya mitambo Saba ya awamu ya kwanza  imeshafungwa shambani hapo huku Mitambo mingine mitatu ikiendelea Kufungwa.

 

Dkt Sophia alisema ifikapo mwishoni mwa mwezi Juni ama mwanzoni mwa mwezi Julai tayari kazi ya Umwagiliaji itaanza kwa Hekta 200 za awali huku hekta 200 nyingine zikiendelea kufungwa mitambo mingine Saba ya awamu ya pili. Hii itafanya jumla ya mitambo 14 katika eneo lote la hekta 400.

 

Alisema kazi hiyo vilevile inaendelea katika mashamba ya Msimba Kilosa Mkoani Morogoro na Arusha Ngaramtoni kazi zinaendelea ambapo Kila Shamba linawekewa umwagiliaji wa hekta 200 na kazi zimefikia asilimia 50.

 

Aliitaka Kampuni hiyo ya Pro Agro Global ltd kufanya kazi Kwa bidii Kwa kujituma na kutanguliza uzalendo ili miradi hiyo iweze kukamilika kwa muda na kudumu kwa muda mrefu na kutoa tija Kwa jamii.

 

Aliwataka watumishi wote waliopo maeneo ya mradi hasa  Technicians wenye taaluma ya umwagiliaji na wahandisi wa umwagiliaji ambao wote wameajiriwa hivi karibuni wahakikishe Wanajifunza Kwa bidii kazi nzima ya ufungaji wa mitambo hiyo Ili kuhakikisha wanaimudu mapema kabla mkandarasi hajakabidhi mradi.

 

Shamba la Mbegu Kilimi Nzega Tabora linazalisha mbengu za mazao mchanganyiko kama vile Mahandi,Alizeti ,Choroko ,Mtama na mihongo shamba ambalo  linalima mazao mchanganyiko .


mwisho

 

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages