Breaking

Thursday 13 July 2023

JAMII YATAKIWA KULINDA MASUALA YAO BINAFSI WANAPOTUMIA MITANDAO YA KIJAMII

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

JAMII imetakiwa kulinda masuala yao binafsi pindi wanapokuwa wanatumia mitandao ya Kijamii ili kuepukana na matendo ya ukatili wa kijinsia ambayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara.

Akizungumza jana Julai 12,2023 katika Semina za Jinsia na maendeleo (GDSS) TGNP Jijini Dar es Salaam, Mwezesha wa Semina Mwl.Dotto Yotham amesema watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii wamekuwa wakikumbwa na vitendo vya ukatili kutokana na mambo yao binafsi kuruhusu kila mtu kuyafahmu.

"Wengi wamekuwa hawana elimu ya hii, tukizungumzia kwenye mtandao wa Facebook, mtu anakuja kukuomba urafiki, haumfahamu, wewe bila kumchungumza na kumfahamu, unamkubalia na ukishamkubia unampa mwanya wa kukufuatilia kwa urahisi na kuweza kupata mwanya wa kukuzalilisha kwa maana inakuwa rahisi kuyajua mambo yako". Amesema Bw.Yotham.

Amesema watumiaji wa mitandao ya kijamii pamoja na simu janja wanatakiwa kuhakikisha wanaweka maneno ya siri (pasword) ambayo ni ulinzi kwa vitu vyake binafsi na asiweze kushare neno lake la siri na mtu yeyote kwani anaweza akakutana na vitendo vya ukatili kupitia kwa yule ambaye amemwamini na kuruhusu neno lake la siri kufahamu.



Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages